Marufuku kubeba watoto kwenye Matanki ya mafuta Geita
14 April 2021, 6:52 pm
Na kalechongela:
Wananchi Geita wameiomba serikali ya mkoa wa kupitia kitengo cha usalama barabarani kudhibiti suala na ubebaji wa watoto kwenye matanki ya mafuta kwenye pikipiki.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa Geita wakati wakizungumza na Storm FM nakusema kuwa kumekuwepo na changamoto ya ubebaji wa watoto mbele ya pikipiki hali ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha ya watoto.
Kwa upande wao baadhi ya madereva pikipiki wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kubainisha kuwa mojo kati ya sababu ambayo inasababisha hali hiyo ni sababu za kiuchumi.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabani Mkoa wa Geita RTO Salehe Rajabu Digega amepiga marufuku ubebaji wa watoto mbele ya pikipiki nakwamba atawachukuliwa hatua kali za kisheria baadhi ya madereva pikipiki watakao kiuka maagizo hayo.