Barabara yapewa jina la JPM wilayani Mbogwe Mkoani Geita
30 March 2021, 1:59 am
Mbunge wa jimbo la mbogwe Nikodemas Maganga ameamua kuiita MAGUFULI ROAD barabara ya kilomita 3 inayotengenezwa kpitia fedha zilizotolewa na hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wake katika wilaya hiyo.
Mbunge Maganga Amesema kutokana na mchango mkubwa wa hayati John Pombe Magufuli katika jimbo hilo wataendelea kumkumbuka kwani kuna baadhi ya miradi inayoondelea kutekelezwa ikiwemo miradi ya barabara na afya.
Katika hatua nyingine mbunge Maganga amewaomba watanzani kuendelea kumpa ushirikiano na kumwamini Rais aliepo kwa sasa Mh Samia Suluhu Hassan huku akiwaomba viongozi wote kumuenzi Dkt Magufuli kwa kujitoa na kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wamemuomba Mhe, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kumuenzi hayati Magufuli kwa kukamilisha miradi iliyoanzishwa wakati wa utawala wake.