Wizi wa ajabu wafanyika duka la dawa.
4 January 2023, 8:25 am
Na Adelina Ukugani:
Jeshi la Polisi mkoani Geita limewataka wafanyabiashara kuchukua tahadhari ya watu ambao wanaenda kama wateja kununua bidhaa kwao ili wasiwaingize katika hasara ya kuibiwa ikiwa ni baada ya muuzaji wa duka la dawa kuibiwa na watu walioingia dukani kwake wakijifanya wagonjwa.
Akizungumzia tukio hilo muuzaji wa duka hilo Frola Emmanuel amesema kuwa watu hao walikuwa wawili na baada ya kumfungia ndani waliondoka na kopo ambalo huwekea fedha na kuchukua zaidi ya Elfu 60,000, huku Jirani yake akitoa ushauri kwa wafanyabaishara.
Akizungumza Kwa njia ya simu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita ACP Safia Jongo amesema licha ya kuwa tukio hilo halijalipotiwa polisi lakini kuna haja ya wafanyabiashara kuwa makini na watu wa namna hiyo.