Storm FM

Alalamikiwa kwa kujenga bila kuzingatia mpaka Mwatulole

21 January 2025, 11:39 am

Wananchi eneo ambalo linadaiwa kuwa na malalamiko ya uzio baina ya majirani. Picha na Kale Chongela

Wananchi manispaa ya Geita wakumbushwa kuzingatia mipaka ya viwanja vyao kabla ya kuanzisha ujenzi ili kuondoa changamoto zinazoweza kupelekea migogoro.

Na: Kale Chongela – Geita

Baadhi ya wananchi wakazi wa eneo la Nguzombili mtaa wa Mwatulole kata ya Buhalahala wamelalamikia baadhi ya watu wenye tabia ya kuanzisha ujenzi wa nyumba kiholela bila kuzingatia mipaka.

Rockey Mussa ni mlalamikaji akizungumza na Strom FM ameeleza juu ya suala hilo akimtuhumu jirani yake kwa kutozingatia uzio baina yao wakati wa ujenzi.

Sauti ya mlalamikaji Rockey Mussa
Pichani ni Rockey Mussa akionesha eneo linalojengwa kwa kutozingatia mpaka Picha na Kale Chongela.

Bi. Ester Maige ni jirani yake Rockey Mussa ambaye analalamikiwa akizungumza na Storm FM kwa njia ya simu amesema anashangaa jirani yake huyo kutotaka mazungumzo na yeye badala yake anashtaki tu.

Sauti ya mlalamikiwa Ester Maige

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwatulole Bw. Edward Msalaba amekiri kuwepo kwa mgogoro huo na kubainisha kuwa tayari ameshatoa maelekezo kupitia ofisi yake.

Sauti ya mwenyekiti Edward Msalaba

Afisa ardhi kutoka manispaa ya Geita Bw. Mwizarubi Selestine akizungumza kwa njia ya simu amewataka wananchi kufuata sheria pindi wanapoanza ujenzi ili kuepusha migogoro.

Sauti ya Afisa ardhi Mwizarubi Selestine