Zaidi ya wananchi 1,300,000 kupiga kura mkoani Geita
27 November 2024, 12:25 pm
Leo Novemba 27, 2024 wananchi Tanzania bara wanashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwaajili ya kuchagua viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Na: Ester Mabula – Geita
Zaidi ya wananchi milioni 1 na laki 3 mkoani Geita wanatarajiwa kushiriki katika zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika leo Novemba 27, 2024 Tanzania bara.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela akiwa katika kituo cha kupigia kura cha Nyanza kilichopo kata ya Kalangalala halmshauri ya mji wa Geita asubuhi ya leo ametoa rai kwa wananchi kujitokeza ili kuweza kutimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura kwani mkoa umejipanga vyema kufanikisha zoezi hilo kwa kufikisha vifaa vyote muhimu katika vituo vyote vya kupigia kura
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la upigaji kura katika mtaa wa Nyanza wameeleza matarajio yao kwa watia nia watakaopata ridhaa ya kuwaongoza.
Uchaguzi wa serikali za mitaa umekua ukifanyika kila baada ya miaka mitano tangu mabadiliko ya kikatiba mwaka 1992 yaliyoruhusu ushiriki wa vyama vingi vya kisiasa mbapo kwa mwaka huu utakuwa ni uchaguzi wa sita kufanyika.