Mkurugenzi Geita mji akagua vituo vya uandikishaji
11 October 2024, 2:02 pm
Leo Oktoba 11, 2024 limezinduliwa rasmi zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Na: Kale Chongela – Geita
Mkururgenzi mtendaji wa halmashauri mji wa Geita Ndugu Yefrerd Myenzi amewataka wananchi kutumia siku kumi zilizopagwa kujitokeza na kujiandikisha katika daftari la makazi.
Myenzi amesema hayo baada ya kukagua kituo cha uandikishaji katika mtaa wa Nyanza kata ya Kalangalala mjini Geita leo oktoba 11 akisisitiza kuwa kujiandikisha katika daftari la makazi itamuwezesha mwananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Diwani wa kata ya Kalangalala Prudence Temba amesema miongoni mwa sifa kuu ya kushiriki katika uchaguzi ni kuhakikisha jina la mwananchi limeandikwa kwenye daftari la makazi.
Baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya mji wa Geita ambao wameshiriki zoezi la uandikishaji katika daftari la makazi wamebainisha kuwa nafasi hii ya wao kujiandikisha inawapa wigo mpana wa kuchagua viongozi wanaofaa.