BAKWATA yaibuka na matukio ya utekaji na mauaji nchini
16 September 2024, 6:12 pm
Kutokana na uwepo wa matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa makundi mbalimbali katika jamii yanalaani juu ya matukio hayo ikiwemo viongozi wa dini.
Na Mrisho Sadick:
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA limelaani vikali matukio ya utekaji na mauaji huku likiiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini watu wanaofanya vitendo hivyo nakuwachukulia hatua za kisheria.
Akitoa taarifa ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania kwenye Baraza la Maulid Mkoani Geita lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwaniaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Katibu Mkuu wa BAKWATA Al Haj Nuhu Mruma amesema kwa sasa vitendo viovu nchini vinaendelea kushamiri.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wakazi wa Mkoa wa Geita kuwakemea baadhi ya watu wanaohatarisha amani ya nchi.
Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania Dkt Abubakary Zubeir ameendelea kuwataka watanzania kudumisha amani nakulinda nchi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema serikali ipo macho Juu ya vitendo viovu huku akiwaomba Wananchi kushirikiana na serikali kukomesha vitendo hivyo.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya maulid mwaka huu ni “Maulid na aman zingatia maadili , uchumi , Shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa”