Mwalimu abaka mwanafunzi na kumtishia kumfukuza shule
10 May 2024, 2:03 am
Uwepo wa matukio ya ulawiti na ubakaji huacha hofu na simanzi kwa watoto jambo ambalo baadhi ya wazazi hushindwa kuelewa juu ya hatma za watoto wao katika kutimiza ndoto zao.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Katoro iliyoko Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro mkoani Geita mwenye umri wa miaka 36 anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16 na kisha kumtishia kumfukuza shule iwapo atamwambia mtu jambo hilo.
Mhanga ambaye ni binti mwenyewe ameeleza namna ambavyo tukio hilo limetokea.
Mama mzazi wa binti huyo akizungumza kwa masikitiko juu ya tukio hilo, ameeleza namna ambavyo alimuona binti yake licha ya binti huyo kutomueleza awali juu ya tukio hilo.
Baba mzazi wa binti huyo amesema tukio hilo limewaumiza sana kwani wanapopeleka watoto shule wanaamini walimu ni walezi wa pili na kwamba wanapofanya vitendo hivyo inawakatisha tamaa.
Akithibitisha juu ya tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP. Safia Jongo amekiri kumshikilia mtuhumiwa huyo pamoja na mkuu wa shule hiyo kwa kushindwa kuchukua hatua baada ya kupokea taarifa ya tukio hilo