Familia zinazoishi mazingira magumu zapatiwa msaada
30 April 2024, 3:39 pm
Hali duni ya maisha inayopelekea kukosa mahitaji mbalimbali inatajwa kuwa chanzo cha baadhi ya watoto kushindwa kupata haki ya eleimu kutokana na wazazi kushindwa kumudu gharama na kupelekea ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Kutokana na baadhi ya familia wilayani Chato mkoani Geita kuishi mazingira magumu jambo ambalo linapelekea wazazi na walezi wa familia hizo kuwatumia watoto kufanya shughuli za kiuchumi badala ya watoto kwenda shule, shirika la Compassion International kwa kushirikiana na makanisa ya kikristo wilayani humo wameanza jitihada za kutatua changamoto hizo kwa kuzijengea familia hizo makazi ya kudumu.
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wanufaika wa mradi huo wanaelezea jinsi ulivyosaidia.
Wasimamizi wa vituo vinavyosimamia miradi hiyo wanabainisha mabadiliko chanya kwa familia hizo tangu zianze kupatiwa msaada huo.
Mkuu wa wilaya ya Chato Said Nkumba ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuzidi kusaidia familia zinazoishi katika mazingira magumu.