TBA yawafikia wanageita kwa kutoa elimu katika maonesho ya 6
27 September 2023, 2:12 pm
TBA imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya serikali kwa uaminifu na uadilifu huku Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongeza wigo katika sekta hiyo na kuiruhusu kufanya kazi na mashirika binafsi.
Na Zubeda Handrish- Geita
Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko TBA Fredrick Kalinga, amesema wameshiki katika maoneshoa ya 6 ya kimataifa ya teknolojia ya madini kama wadau wakuu katika uendelezaji wa sekta hiyo kwa kutoa huduma ya ujenzi wa majengo pamoja na nyumba za makazi na kwa upande wa madini wakifanya ubunifu katika jengo lao la ofisi ya madini.
Mkoani Geita pia TBA wamefanya ubunifu wa jengo la Mkuu wa Mkoa na kusimamia ujenzi wake, ubunifu katika majengo yote na kujenga Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, Ofisi ya TANESCO Geita pamoja na ofisi mbalimbali huku wananchi wa maeneo husika wakinufaika katika ushiriki wa ukamilishwaji wa majengo hayo.
Lengo kubwa la TBA katika maonesho haya ni kuwafahamisha wananchi kazi zao huku wakitoa pongezi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuruhusu taasisi hiyo kushirikiana na makampuni binafsi.
Mapema mwezi huu Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa alitembelea Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya katika kutekeleza miradi ya Serikali hususani, ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma.