Idara ya mazingira Geita yaja na mikakati ya kudhibiti taka
1 September 2023, 4:25 pm
Uchafuzi wa mazingira na utupaji taka hovyo katika halmashauri ya mji wa Geita ambapo ndio kitovu cha mkoa, umepelekea idara ya mazingira kuja na mpango mkakati kudhibiti uchafuzi huo.
Na Kale Chongela- Geita
Idara ya Mazingira halmashauri ya mji wa Geita imekuja na mikakati ya kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka ikiwa lengo ni kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi.
Akizungumza na Storm FM Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Mjini Geita Bw. Aloyce Mtayuga amesema vifaa hivyo vimewekwa pembezoni mwa barabara ikiwa ni kuhakikisha, wananchi hawapati usumbufu wa wao kutunza taka ambazo wanajizalisha.
Aidha Bw. Mtayuga ameongeza kwa kusema licha ya uwepo wa vifaa hivyo maalumu kwa ajili ya kutunzia taka, yapo pia magari ambayo ni maalumu kwa ajili ya kubeba taka hizo.