Wananchi zaidi ya laki 6 wanufaika na mradi wa maji Geita
28 August 2023, 9:07 am
Changamoto ya kupatikana kwa maji safi na salama vijijini, imechangia kwa kiasi kikubwa mradi wa maji wa miji 28 kuanzishwa.
Na Adelina Ukugani- Geita
Jumla ya wakazi laki sita na thelathini na nane mia tatu na ishirini na mbili (638,322 ) wanatarajia kunufaika na mradi wa maji wa miji 28 , ambapo jumla ya kata 19 na vijiji 19 vilivyopo Wilayani Geita vinatarajia kupata manufaa ya uwepo wa mradi huo wa maji ambao unajengwa kwenye Kata ya Senga Wilayani humo.
Hii ni baada ya kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kukagua miradi na kufika kwenye eneo ambalo ndipo linatarajia kuanza ujenzi wa mradi huo.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhadisi Isaac Mgeni kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mjini Geita (GEUWASA)ameelezea hatua za awali ambazo wanaendelea nazo.
Diwani wa kata ya Senga Thomas Tumbo, amedai changamoto iliyopo ni wananchi kuthaminiwa na kulipwa fidia kwa wale ambao mashamba yao yatapitiwa na mradi.
Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Geita, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilayani Humo, Taitus Kabuo amesisitiza ni vyema kwa fidia ikafanywa haraka ili iweze kulipwa kwa wananchi ambao mradi utawapitia.
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita, imefanya ziara katika wilaya mbalimbali mkoani hapa na kufanya ukaguzi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.