Miradi ya bilioni 5.6 yakutwa na mapungufu
10 August 2023, 6:18 pm
Vitendo vya rushwa vimeendelea kuwa na athari kubwa hadi kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa ajili ya wananchi.
Na Mrisho Sadick:
Miradi 12 yenye thamani ya shilingi Bilioni 5.6 imebainika kuwa na Mapungufu na viashiria vya rushwa wakati wa utekelezaji wake mkoani Geita.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Geita Leonidas Felix wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari ya utekelezaji wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia April had juni mwaka huu ambapo amesema jumla ya miradi 33 yenye thamani bilioni 16 .8 imefuatiliwa.
Aidha amesema katika kipindi hicho cha April hadi Juni mwaka huu tasisi hiyo imetoa elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa kwa makundi mbalimbai ili kuhamasisha UMMA Kuendelea kushiriki mapambano dhidi ya Rushwa ambapo jumla ya kazi 31 za uelimishaji zimefanyika .
Hata hivyo ameongeza kuwa kero 168 ziliibuliwa kupitia vikao vya makundi hayo na kati ya kero hizo zimeanza kutatuliwa ikiwemo kuwatafuta walengwa ili kujibu malalmiko hayo.