Miradi 59 ya bilioni 29 kuzinduliwa na mwenge wa uhuru mkoani Geita
2 August 2023, 11:52 pm
Mwenge wa Uhuru umeanza kukimbizwa mkoani Geita Agosti 02,2023 na utakimbizwa kwa siku sita katika halmashauri sita za mkoa huo kisha kukabidhiwa Agosti 08 mwaka huu mkoani Kagera.
Na Mrisho Sadick:
Wakazi zaidi ya Eefu nane (8,000) wa kijiji cha Bulangale wilayani Nyang’hwale mkoani Geita wameondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji baada ya Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA wilayani humo kutekeleza mradi wa maji wenye thamani ya shilingi bilioni moja.
Mradi huo wa maji wenye tenki lenye ujazo wa lita laki moja umetembelewa na mbio za mwenge wa uhuru ambazo zimeanza kukimbizwa mkoani Geita na taarifa ya mradi huo ikasomwa na meneja wa RUWASA wa wilaya ya Nyang’hwale Mhandisi Moses Mwampunga .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdallah Shaib Kaimu baada ya kutembelea mradi huo ameridhishwa na utekelezaji wake.
Awali akiupokea mwenge wa uhuru kutoka mkoani Shinyanga mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema mwenge wa uhuru ukiwa mkoani Geita utakimbizwa kilomita 755 na utapitia miradi 59 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 29 katika halmashauri sita za mkoa wa Geita.