TAKUKURU Geita yaokoa zaidi ya shilingi milioni 11
1 August 2023, 10:45 pm
Wakulima wa pamba wamelalamikia kutapeliwa pesa zao za mauzo, hali iliyopelekea TAKUKURU kuingilia kati.
Na Kale Chongela- Geita
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Geita imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi Milioni 11 zilizokuwa zimetapeliwa na viongozi wa chama cha msingi cha Nyakalemba cha wilaya ya Nyangh’wale mkoani Geita kutoka kwa wakulima 22 wa vijiji vya Kasubaya na Igeka wilaya humo.
Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wakulima wa zao la pamba katika vijjiji vya Kasubaya na Igeka wilayani Nyanghwale mkoani Geita wamesema baada ya kuvuna pamba yao walienda kuuza kwenye chama cha msingi cha Nyakalemba kilichopo wilayani humo tarehe 09 Septemba 2022 lakini hawakupatiwa fedha hizo hadi pale walipoamua kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya kuomba usaidizi wa kulipwa fedha zao.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Leonidas Felix amesema baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo alifanikiwa kurejesha fedha hizo na zikarudishwa kwa wakulima hao.