Timu 21 kushiriki ligi daraja la 3 Geita
17 July 2023, 10:51 am
Kila mwaka mashindano ya Ligi daraja la tatu yanafanyika kwa maandalizi makubwa na matarajio ya kuikuza Ligi hiyo mkoani Geita, huku moja ya changamoto ikiwa ni kucheleweshwa kuwasilisha bingwa wa wilaya kwa vilabu.
Na Amon Bebe- Geita
Ligi Daraja la tatu mkoa wa Geita inatarajia kuanza rasmi mwezi wa nane.
Hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa kamati ya mashindano mkoa wa Geita Baraka Ramadhani hapo jana kwenye kikao kilichofanyika Ofisi za Chama cha Soka mkoa wa Geita GEREFA, ambapo amesema Ligi hiyo itashirikisha timu 21 msimu huu na tayari fomu za ushiriki zipo na zinaanza kutolewa leo kwa vilabu shiriki.
Kwa upande wa Katibu wa kamati ya mashindano mkoa wa Geita Gijeta Jackson amevikumbusha vilabu shiriki kuchukua fomu mapema na kuvihakikishia kuwa Ligi ya msimu huu itakuwa na ubora mkubwa tofauti na miaka ya nyuma.