Imani ni kubwa kwa Taifa Stars kufuzu
16 July 2023, 3:58 pm
Ili Stars iweze kufuzu Kombe la Dunia 2026, inatakiwa kutorudia makosa ya nyuma kwa kuandaa kikosi mapema ikizingatiwa kuandaa mashindano ya vijana kwa wingi, na ndilo hasa lilowaibua wadau.
Na Zubeda Handrish- Geita
Baada ya Droo ya hatua ya awali ya Kufuzu Kombe la Dunia la FIFA 2026 kufanyika Alhamisi, Julai 13, 2023 mjini Abidjan, Ivory Coast, na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kupangwa kundi E hoja zikaibuka juu ya kufuzu kushiriki Kombe hilo.
Tanzania katika kundi lake imepangwa na Morocco, Zambia, Congo, Niger na Eritrea, na ndicho hasa kilichoibua hoja huku ikidaiwa kundi hilo ni gumu kiasi na rahisi kiasi.
Mashabiki wa soka kutoka mtaa wa Mwatulole uliopo kata ya Buhalahala, wilayani na mkoani Geita wamezungumzia ugumu na urahisi wa kundi hilo huku zaidi wakijipa moyo maandalizi yakiwa ya mapema basi Taifa Stars itafuzu Kombe la Dunia 2026.
Washindi 9 wa kila kundi watafuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia 2026 huku timu nne zinazofuata kwenye msimamo wa kila kundi (best loosers) zikitarajiwa kufuzu hatua ya mchujo ya mabara (inter-continental playoff)