Shigela: Viongozi wa dini wana mchango mkubwa katika amani ya nchi
14 July 2023, 1:28 pm
Inaelezwa kuwa utulivu , amani , umoja na mshikamano katika taifa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa dini kuendelea kuwajenga kiimani wananchi.
Na Kale Chongela:
Serikali mkoani Geita imesema inatambua mchango wa viongozi wa dini katika kuleta umoja na amani nchini nakuahidi kuendelea kuwaunga mkono katika shughuli zao zakufikisha neno la mungu kwa wananchi.
kauli imetolewa na mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela katika uzinduzi wa mkutano wa Injili wa kanisa la Efatha, katika uwanja wa CCM Kalangalala mjini Geita.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishna msaidizi wa Polisi ACP Safia Jongo amesema uwepo wa mikutano ya Injili utasaidia watu kuendelea kujifunza mafundisho mema nakuacha matendo mauvu.
Kwa upande wake Mtume Nabii Josephat Mwingila amesema injili ndo msingi Mkubwa wa mafanikio nakwamba ni vyema kila mmoja amjue mungu kuwa ndye mwokozi wa maisha yeke.