Storm FM

Geita ni shwari kuelekea sikuku – SACP Jongo

24 December 2025, 7:16 pm

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Picha na Ester Mabula

Kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita atoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu wakati wa kusheherekea.

Na: Ester Mabula

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Geita kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa amani na utulivu huku akiwasihi wazazi na walezi kuwalinda watoto wao.

Ametoa rai hiyo leo Disemba 24, 2025 akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema Jeshi la polisi mkoa wa Geita limejpanga vyema kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yote ya mkoa.

Sauti ya kamanda wa polisi Geita SACP Safia Jongo
Eneo la kuingia ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo. Picha na Ester Mabula

Aidha amewasihi wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao katika kipindi hiki ili kuondoa changamoto za ukatili zinazoweza kuwapata watoto.

Sauti ya kamanda wa polisi Geita SACP Safia Jongo

Katika hatrua nyingine amewakumbusha watumiaji wa vyombo vya moto hususani madereva kuwa makini wakati wanapotumia barabara ili kuepusha ajali za barabarani,

Sauti ya kamanda wa polisi Geita SACP Safia Jongo
Bango la mwelekeo wa ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Geita. Picha na Ester Mabula