Storm FM

Mchakato ulipaji fidia eneo la GGML waanza

25 November 2025, 2:56 pm

Mthamini mkuu wa serikali Bi. Everne Mgasha akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Edga Rwenduru

Ni zaidi ya miezi miwili sasa tangu agizo la serikali kupitia wizara ya madini kuelekeza malipo ya fidia kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa GGML.

Na: Edga Rwenduru

Hekari 2790 kati ya Hekari 3900 za ardhi tayari zimefanyiwa uthamini kwa ajili ya kuwalipa Fidia wananchi waishio katika leseni ya Mgodi wa GGML ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la serikali la kuwalipa na kuwaondoa wananchi hao ili shughuli za uchimbaji madini ziendelee kufanyika katika maeneo hayo.

Hayo yameelezwa na Mthamini mkuu wa serikali Bi. Everne Mgasha wakati akiwa mkoani Geita kwaajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mvua zilizonyesha mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ambayo yanatarajiwa kulipwa fidia kwa wananchi.

Sauti ya Everne Mgasha, mthamini mkuu wa serikali
Zoezi la kukagua eneo linalofanyiwa uthamini kwaajili ya malipo ya fidia. Picha na Edga Rwenduru

Aidha Bi. Everne Mgasha ameongeza kuwa katika zoezi hilo wamekumbana na changamoto kubwa ya tegesha na baadhi ya nyumba kuangushwa na mvua kabla ya zoezi la uthamini kuanza.

Sauti ya Everne Mgasha, mthamini mkuu wa serikali

Lwitiko Bukuku ni mthamini kutoka kampuni ya Widenights amesema mpaka sasa wamefikia zaidi ya asilimia 90% ya ukaguzi wa mali shambani.

Sauti ya Lwitiko Bukuku kutoka kampuni ya Widenights
Mthamini kutoka kampuni ya Widenights Lwitiko Bukuku akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Edga Rwenduru