Storm FM

Nyan’ghwale iko shwari kuelekea uchaguzi kesho

28 October 2025, 11:13 am

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita Grace Kingalame akizungumza na Storm FM. Picha na Mrisho Sadick

Idadi ya wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni wilayani Nyang’hwale 124,036 na kuwa jumla ya vituo 360.

Na Mrisho Sadick:

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Grace Kingalame, amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kuwa hali ya usalama kuelekea uchaguzi mkuu iko shwari, huku akiwataka wote waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi.

Kingalame amebainisha hayo ofisini kwake wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema idadi ya wananchi waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ni 124,036 na kuwa jumla ya vituo 360 vya kupigia kura vimeandaliwa kuhakikisha kila mpiga kura anatimiza haki yake kwa wakati.

Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa chama cha mapinduzi. Picha na Mrisho Sadick

Katika hatua nyingine Kingalame amesema mwitikio wa Wananchi kufuatilia sera za wagombea mbalimbali wakati wa mikutano ya kampeni ulikuwa mkubwa hivyo Oktoba 29 watakwenda kufanya maamuzi baada ya kupima sera hizo.

Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa chama cha ADA TADEA. Picha na Mrisho Sadick

Baadhi ya wananchi wilayani humo wamesema wamejiandaa kikamilifu kushiriki uchaguzi mkuu kwakuwa wamepima sera za wagombea wote waliopita kwenye maeneo yao kunadi ilani zao.