Storm FM
Storm FM
24 October 2025, 6:03 pm

Zimesalia siku 4 ili wananchi nchini waweze kushiriki haki ya msingi na ya kikatiba ya kupiga kura kuchagua madiwani, wabunge na Rais.
Na: Ester Mabula
Mgombea Udiwani wa kata ya Kalangalala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Reuben Sagayika leo Oktoba 24, 2025 ametembelea wananchi katika maeneo yao ya kazi na kuzungumza nao juu ya fursa na changamoto zinazowakabili.
Amezungumza na wajasiriamali sokoni, wafanyakazi wa garage na wananchi wa kawaida ambao wamemueleza changamoto zinazowakabili.
Sagayika ameahidi iwapo watamchagua atafanya kazi kwa kushirikiana nao akiahidi mazingira bora ya kufanyika kazi, kusaidia fursa za ujasiriamali akisisituza kuwa lengo lake ni kubadili maisha ya wakazi wa kata hiyo akiwa na kaulimbiu isemayo “Uongozi wa uwazi, maisha bora kwa wote”






