Storm FM

Jeshi la Polisi lasema Geita kapigeni kura hakuna wakuwagusa

20 October 2025, 6:05 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita akizungumza na wakazi wa Kata ya Senga wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Wakati zikiwa zimesalia siku nane kuelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba 29,2025 jeshi la polisi Geita lawatoa hofu wananchi.

Na Mrisho Sadick:

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limewahakikishia Wananchi wa Mkoa huo usalama wa kutosha wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 29 huku likiwataka kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kupiga kura.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo akizungumza na wakazi wa Kata ya Senga wilayani Geita amewaondoa hofu Wananchi Juu ya kile kinachoendelea kwenye mitandao ya Kijamii akisema Jeshi hilo limejipanga kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wakazi wa Kata ya Senga wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wananchi Mkoani Geita kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwakuwa hakuna Mtu yoyote mwenye uwezo wa kuwazuia kutimiza haki yao.

Sauti ya ripoti ya stori hii