Storm FM
Storm FM
6 October 2025, 7:41 pm

“Ninaimani kata ya Kalangalala itakwenda kubadilika kimaendeleo iwapo mtanipa kura za NDIO ili niweze kuwatumikia kwa moyo wangu” – Reuben Sagayika
Na: Ester Mabula
Mgombea udiwani wa kata ya Kalangalala kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Reuben Sagayika leo Oktoba 06, 2025 ameendeleza kampeni za kunadi sera zake na ilani ya CCM ambapo amezungumza na wakazi wa eneo la Msufini kata ya Kalangalala, halmashauri ya manispaa ya Geita.
Katika mkutano huo Sagayika amewaomba wakazi wa kata ya Kalangalala na wananchi kwa ujumla kuchagua viongozi watokanao na CCM katika ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais ili kuleta maendeleo kwa Jamii.

Akizungumza mbele ya Mgombea Ubunge wa jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Wambura ametoa maombi matatu ambayo ataanza nayo katika utatuzi wa changamoto iwapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kwa kuzingatia makundi ya vijana, wanawake pamoja na wazee.
