Storm FM

Njema Labs sasa kutoa huduma kwa wananchi saa 24

25 September 2025, 4:49 am

Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipotembelea banda la Njema Labs baada ya kuzindua rasmi maonesho ya madini. Picha na Mwandishi wetu

Maonesho ya madini ya Geita ni sehemu ya juhudi za serikali kupitia wizara ya madini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, katika kuendeleza sekta ya madini kwa kutoa elimu, kukuza ushirikiano wa kibiashara na kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wachimbaji na wananchi kwa ujumla.

Na: Ester Mabula

Kampuni ya Njema Laboratory (Njema Labs) inayojihusisha na upimaji wa sampuli za madini imepongeza uwepo wa maonesho ya madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu eneo la Bombambili manispaa ya Geita kwani yanarahisisha watu kupata huduma mbalimbali kwa urahisi na haraka.

Akizungumza na Storm FM Septemba 24, 2025 akiwa katika maonesho hayo mwakilishi wa kampuni hiyo Bi. Evelina Felix Nkoko ameeleza kazi na shughuli mbalimbali wanazofanya kupitia Njema Labs na kuwakaribisha wananchi kutembela katika banda lao kwa huduma bora zaidi.

Sauti ya Adelina Felix Mkoko kutoka Njema Labs
Bi. Adelina Felix Mkoko akizungumza na mwandishi wetu (hayupo pichani) akiwa katika banda la Njema Labs. Picha na Ester Mabula

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bw. Emmanuel Solomon amesema kupitia ushiriki wao katika maonesho hayo wanatoa  kutoa elimu ya bure kuhusu umuhimu wa kupima sampuli, taratibu za upimaji, pamoja na viwango vinavyotakiwa katika soko la ndani na la kimataifa na kueleza kuwa kwa sasa wako mbioni kutoa huduma kwa wanachi kwa saa 24

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Njema Labs Emmanuel Solomon
Mkurugenzi mtendaji wa Njema Labs Bw. Emmanuel Solomon akifafanua jambo juu ya huduma zao. Picha na Ester Mabula

Njema Labs ni miongoni mwa kampuni za ndani zinazochipukia kwa kasi katika sekta ya huduma za maabara ya madini, na imeweka msukumo mkubwa katika kuhakikisha wachimbaji wanapata huduma bora kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Tuzo waliyokabidhiwa mwaka 2024 katika maonesho hayo ya mshindi wa tatu, kampuni wezeshi kwenye sekta ya uchimbaji. Picha na Ester Mabula