Storm FM
Storm FM
18 September 2025, 7:38 pm

Storm FM imekuwa daraja la kuunganisha jamii ya Geita kupitia vipindi vyake vya elimu, michezo, habari na burudani, jambo ambalo limewasaidia kuongeza mshikamano.
Na Boaz Azalia:
Wananchi mkoani Geita wameipongeza Storm FM kwa kutimiza miaka 11 leo tangu ianze kurusha matangazo yake mnamo tarehe 18 Septemba 2014.
Wamesema kituo hiki cha redio kimekuwa sehemu muhimu ya maisha yao kwa kutoa taarifa sahihi na burudani inayogusa jamii kwa ukaribu mkubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wamesema Storm FM imekuwa chachu ya maendeleo kwani imekuwa ikiibua changamoto zinazowakabili na kuzifikisha kwa mamlaka husika, hatua ambayo imechangia kupatikana kwa ufumbuzi katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Aidha, wameeleza kuwa redio hiyo imekuwa daraja la kuunganisha jamii ya Geita kupitia vipindi vyake vya elimu, michezo, habari na burudani, jambo ambalo limewasaidia kuongeza mshikamano.
Hata hivyo, wananchi hao wameitaka Storm FM kuendelea kujiboresha zaidi ili iendelee kuwa sauti ya jamii na kuimarisha nafasi yake kama chombo cha habari kinachojali maendeleo ya wananchi kwa ujumla.