Storm FM
Storm FM
12 September 2025, 4:34 am

Tanzania inajiandaa na Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 ambapo rai imetolewa kwa wasimamizi wa uchaguzi kuepuka vitendo vya Rushwa.
Na: Edga Rwenduru
Taasisi ya kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Geita imewaonya wananchi na wasimamizi wa uchaguzi watakaobainika kugushi nyaraka za uchaguzi kwa lengo la kuwatafutia ushindi baadhi ya wagombea.
Akizungumza Septemba 11, 2025 wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na TAKUKURU kwa wasimamizi wa uchaguzi mkoa wa Geita, Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Geita Said Lipunjaje ambaye alikuwa ni mwezeshaji mada katika warsha hiyo amesema TAKUKURU wapo makini kufatilia wasimamizi ambao watakiuka maadili.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita James Ruge amesema Taasisi hiyo inalenga kufikisha elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa kwa wananchi katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Nao baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi walioshiriki katika warsha hiyo wamesema wapo tayari kutekeleza maelekezo yote waliyopewa na TAKUKURU ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru na haki.
