Storm FM
Storm FM
22 August 2025, 1:16 pm

Ujenzi wa maabara ya madini Geita ni miongoni mwa maabara za utafiti wa madini kubwa tatu zinazojengwa nchini Tanzania
Na: Ester Mabula
Kutokana na changamoto ya wachimbaji wa madini kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kusafiri umbali mrefu hadi Dodoma kwaajili ya kupata huduma ya utafiti wa madini, serikali imeanza ujenzi wa maabara kubwa ya utafiti wa madini mkoani Geita itakayohudumia zaidi ya mikoa sita ya kimadini kanda ya ziwa.
Ujenzi wa maabara hiyo unafanyika katika kata ya Kanyala manispaa ya Geita ambapo Waziri wa madini Mhe. Anthony mavunde ametembelea eneo hilo Agosti 21, 2025 na kueleza ujenzi huo ni utekelezaji wa ahadi ya serikali ya kujenga maabara kubwa tatu nchini.
Akizungumza Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde mara baada ya kutembelea eneo hilo amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kutimiza ahadi zake katika maeneo yanayojihusisha na shughuli za madini.

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela amesema ujenzi wa maabara hiyo ukikamilika utakuwa msaada mkubwa kwa wachimbaji madini kwani itawapunguzia gharama za uendeshaji.
Nokita Benteze ni Mkurugenzi wa huduma za maabara GST amesema ujenzi wa maabara hiyo utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.5 ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 390.
