Storm FM

Warundi 39 wakamatwa katikati ya pori Geita

12 August 2025, 2:15 pm

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Geita akizungumza na rai wa Burundi waliokamatwa Geita. Picha na Mrisho Sadick

Katika oparesheni hiyo wamekamatwa watanzania wawili mmoja alikuwa amepangisha baadhi ya raia hao wa kigeni.

Na Mrisho Sadick:

Raia wa Burundi 39 wakiwemo waliovamia pori la akiba la Mshinde nakuanzisha shughuli za kilimo wilayani Geita mkoani Geita wamekamatwa na idara ya uhamiaji katika mwendelezo wa opareshemi zake za kuwasaka nakuwakamata wahamiaji wote walioingia nchini kinyume cha sheria.

Idara ya Uhamiaji mkoani Geita katika oparesheni zake za kukabiliana na wimbi la raia wa kigeni wanaoingia nchini bila kufuata utaratibu imeendelea kuwa na mafanikio makubwa kutokana na idadi kubwa ya raia hususani wa Burundi kukamatwa nakurejeshwa makwao.

Naibu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Geita akizungumzia kukamatwa kwa rai wengine wa Burundi Geita. Picha na Mrisho Sadick

Naibu afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Geita Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Donald Lyimo amesema raia waliokamatwa katika oparesheni hiyo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye pori la akiba la Mshinde ni 39 , Wanaume 24, Wanawake 3 na Watoto 12.

Sauti ya Naibu Afisa Uhamiaji Geita
Miongoni mwa watoto raia wa Burundi waliokamatwa katika oparesheni hiyo Mkoani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Lyimo amesema Katika oparesheni hiyo wamewakamata watanzania wawili mmoja alikuwa amewapangisha baadhi ya raia hao na mwingine alikuwa akiwatumikisha kwenye shughuli za kilimo.

Sauti ya Naibu Afisa Uhamiaji Geita

Sababu za rai hao kuvuka mipaka nakuingia nchini Tanzania ni kutafuta maisha bora kwa madai kuwa katika taifa lao kuna changamoto za kiuchumi na usalama.

Sauti ya raia wa Burundi