Storm FM
Storm FM
5 August 2025, 6:39 pm

Katika oparesheni hiyo watanzania watano wamekamatwa kwa kuwatumia raia hao wa kigeni kinyume cha Sheria.
Na Mrisho Sadick:
Idara ya Uhamiaji Mkoani Geita katika Oparesheni zake imefanikiwa kuwakamata raia 20 wa Burundi walioingia nchini kinyume cha sheria nakufanya idadi ya raia wa kigeni waliokamatwa kwa kipindi Cha miezi miwili kufikia 331.
Naibu Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Geita Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Donald Lyimo amesema raia hao wanadaiwa kuingia nchini kwa lengo la kutafuta ajira hasa kwenye mashamba ya kilimo cha mananasi yaliyopo katika maeneo ya wilaya ya Geita vijijini nakwamba raia hao 20 waliokamatwa mwezi huu 19 kutoka Burundi na 1 kutoka Uganda.

Lyimo amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Agosti 04,2025 wamefanikiwa kuwakamata nakuwarejesha nchini kwao raia wa kigeni 331 kutoka mataifa ya Burundi 312, Rwanda 14,DRC Kongo 4 na Uganda 1 ambapo wengi wamekiri kuvuka mipaka bila vibali maalum nakwamba katika oparesheni hiyo watanzania watano wamekamatwa kwa kuwatumia raia hao wa kigeni kinyume cha Sheria.

Raia waliokamatwa Hechezenabena Beliti na Paschal Kulababuma wameeleza kuwa sababu kuu ya kuvuka mipaka ni kutafuta maisha bora kutokana na changamoto za kiuchumi na usalama katika nchi zao, hata hivyo Idara ya Uhamiaji Mkoani Geita imesisitiza kuwa itaendelea na oparesheni hizo ili kulinda usalama wa taifa na kuhakikisha sheria za uhamiaji zinafuatwa ipasavyo.