Storm FM

Msako waganga wanaobaka wateja wao Geita

27 May 2025, 12:58 pm

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Safia Jongo Safia Jongo akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyakagomba. Picha na Mrisho Sadick

Waganga matapeli wadaiwa kuongezeka kwa kasi Geita jeshi la polisi lakaa mkao wa kula kuwasaka nakuwachukulia hatua.

Na Mrisho Sadick:

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limeanza msako wa kuwatafuta baadhi ya waganga wa jadi katika Kata ya Nyakagomba wilayani Geita wanaodaiwa kuwalaghai wanawake wanaokwenda kutafuta huduma kwao kwa kuwalewesha nakuwaingilia kimwili bila idhini yao kisha kuwarekodi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Safia Jongo wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyakagomba katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo amesema mbali na waganga hao kuwafanyia ukatili huo wamekuwa wakiwarekodi kisha kuwatishia kuwaua au kusambaza picha hizo endapo watakwenda kuripoti.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Geita

Katika Ziara hiyo wakazi wa Kata hiyo akiwengo Jemeremia Mwendamkono wameiomba serikali kuwawekea Transformer yenye uwezo wa kuendesha viwanda vya kuchakata mpunga kwakuwa iliyopo kwasasa inashindwa kuhimili huku kaimu meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Mhandis Michael Mbwana amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo nakwamba katika bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 wanatakwenda kuondoa changamoto hiyo.

Sauti ya Wananchi na Meneja wa TANESCO

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na wananchi hao amewahakikishia kuwa serikali itafanyia kazi changamoto hiyo pamoja nakufikisha Nishati hiyo kwenye kila  kitongoji Cha Kata hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyakagomba. Picha na Mrisho Sadick

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa katika Kata hiyo mbali nakuzungumza na Wananchi ametembelea ujenzi wa mradi wa bwalo la chakula katika shule ya sekondari Butundwe lililojengwa kwa thamani ya zaidi ya Milioni 366 kwa fedha za (CSR).