Storm FM
Storm FM
3 May 2025, 2:28 pm

Licha ya Jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kuelimisha watumiaji wa vyombo vya moto kuepuka mwendo kasi, bado ni changamoto kwa baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto.
Na: Kale Chongela:
Madereva pikipiki waliopo Njia panda ya Mgusu katika halmashauri ya Manispaa ya Geita wamedai kukerwa na tabia ya madereva wa magari makubwa yanayosomba udogo unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu kwa kuendesha mwendo kasi.
Baadhi ya madereva pikipiki wakiwa eneo hilo wameiambia Storm FM kuwa endapo changamoto hiyo kama haitotatuliwa inaweza kusababisha ajali kwani eneo hilo hukutanisha watu mbalimbali kwaajili kufanya shughuli za kujikwamu kiuchumi.
Mwenyekiti wa madereva pikipiki kanda ya Mgusu Juma Nyamsuka amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kwamba suala hilo linatakiwa kutatuliwa kabla ya kusababisha ajali.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabara mkoa wa Geita Mrakbu wa Polisi Aloyce Jacob akizungumza kwa njia ya simu amesema madereva ambao wanavunja sheria za usalama barabaria ikiwemo kuendesha mwendo kasi hawatafumbiwa macho na kuahidi kutatua changamoto hiyo kwa kuwachukulia hatua.
