Storm FM

UVCCM mkoa wa Geita wapewa mafunzo ya uongozi

15 February 2025, 4:09 pm

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika mafunzo ya uongozi kwa UVCCM mkoa wa Geita.

Vijana wa UVCCM mkoa wa Geita wametakiwa kujiamini na kupambania nafasi mbalimbali za kiuongozi kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.

Na: Ester Mabula – Geita

Kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu, Vijana wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Geita wametakiwa kuacha kujipa nafasi ya upambe kwa wagombea na badala yake wachangamkie nafasi hizo wao wenyewe.

Wito huo umetolewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Gervas Evarist wakati akifungua mafunzo kwa viongozi mbalimbali wa umoja huo kutoka wilaya zote za mkoa wa Geita yaliyoandaliwa na mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Geita Manjale Magambo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa CCM Taifa ambae ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa katika kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa CCM lakuwataka vijana wa umoja huo kujengewa uwezo.

Sauti ya MNEC Gervas Evarist
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Gervas Evarist. Picha na Ester Mabula.

Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita Manjale Magambo amesema wakufunzi wa mafunzo hayo wametoka katika kada mbalimbali ikiwemo idara ya Organization makao makuu na kwamba  mwaka huu umoja huo umepanga kuweka historia ya vijana wengi  kuwania nafasi za uongozi katika vyombo vya kutoa maamuzi ikiwemo Udiwani na Ubunge.

Sauti ya mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita Manjale Magambo
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Geita Manjale Magambo. Picha na Ester Mabula.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Geita Bi. Naomi Fujo na Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Nyang’wale Enock Kaswahili wamesema wanaamini UVCCM ni Jumuiya inayojenga vijana na kuwakuza vyema kwaajili ya kulitumikia Taifa.

Sauti ya viongozi wa UVCCM wilaya ya Geita na Nyangh’wale
Vijana wa UVCCM mkoa wa Geita wakiwa katika mafunzo ya uongozi. Picha na Ester Mabula.