

13 February 2025, 10:37 am
Storm FM imemtafuta Kamanda wa polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo juu ya wimbi la wizi wa mifugo aina ya ng’ombe ambao umeendelea kushamiri mkoani Geita.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo ametoa taarifa juu ya matukio ya wizi wa mifugo aina ya ng’ombe ambayo kwa siku za hivi karibuni yameendelea kujitokeza mkoani Geita.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa Februari 12, 2025 ameeleza kuwa Jeshi la polisi limeendelea na jitihada za kupambana na matukio hayo na kwamba mara nyingi watu wanaotenda hivyo ni wafungwa waliohukumiwa hapo awali kwa makosa hayo na baada ya kuachiwa huru wamekuwa wakiendelea kutenda uhalifu huo.
Pia, Kamanda Jongo amesisitiza kuwa kazi ya kupambana na wizi wa mifugo itaendelea, huku akitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Geita kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu ili kudumisha amani na usalama.