Storm FM

Madiwani wampongeza Rais Samia, Geita mji kuwa Manispaa

10 February 2025, 2:36 pm

Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha baraza kilichoketi Februari 07, 2025. Picha na Ester Mabula

Mkutano wa baraza la madiwani umefanyika kwaajili ya uwasilishaji wa changamoto mbalimbali pamoja na mapitio ya utekelezaji miradi kwa kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Disemba 2024.

Na: Ester Mabula – Geita

Baraza la madiwani la Geita mjini limepongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya kuupandisha hadhi mji wa Geita na kuwa halmashauri ya Manispaa.

Hayo yamebainishwa Februari 07, 2025 katika kikao cha baraza la madiwani cha utekelezaji wa miradi kwa robo ya pili kuanzia Oktoba hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Geita Yefred Myenzi. Picha na Ester Mabula

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Geita Yefred Myenzi amesema hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya mji na inaonyesha juhudi za serikali katika kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.

Sauti ya mkurugenzi manispaa ya Geita Yefred Myenzi

Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole amesema kuwa hatua hiyo ni kielelezo cha kupiga hatua kimaendeleo huku akipiingeza serikali ya aawamu ya sita kwa kuwaongezea walimu 48, huku madiwani wengine wakipongeza hatua hiyo.

Sauti ya madiwani
Kaimu Meya manispaa ya Geita na Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole. Picha na Ester Mabula

Mwenyekiti wa CCM wilaya Geita Barnabas Mapande ameeleza kuwa dhamira ya serikali ni kuendelea kuchochea maendeleo nchini huku  Msahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Geita Mhe. Costantine Morandiakiungana na madiwani wenzake kumpongeza na kumshukuru Rais kwa hatua hiyo.

Sauti ya mwenyekiti CCM wilaya ya Geita na Mstahiki Meya