

6 February 2025, 4:00 pm
“Wezi wametuchosha tutaendelea kuwatandika viboko ili waache kutuibia mali zetu” – Mwananchi
Na: Amon Mwakalobo – Geita
Mwananume mmoja mwenye umri wa miaka 36 aliyejitambulisha kwa jina moja la Omary mkazi wa mtaa wa Mission halmashuri ya manispaa ya Geita ameambulia kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kutoka mtaa wa Msalala road baada ya kukutwa akiiba kuni kwa mwanamke mmoja mkazi wa mtaa huo.
Akizungumza na Storm FM mmiliki wa kuni hizo amesema aliambiwa na jirani yake aliyemuona akiiba na ndipo akamkamata na kumpeleka ofisi ya Setikali ya Mtaa, huku akisema amekuwa akiibiwa kuni zake mara kwa mara.
Mtuhumiwa Omary amesema ni mara ya kwanza kuiba kuni hizo hivyo akaomba msamaha huku akiahidi kutorudia tena kuiba.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo amesema wamechoshwa na tabia za wezi katika mtaa huo,na kuwaonya wezi waache tabia hiyo.
Kamanda mkuu wa sungusungu mtaa wa Msalala road Tumaini Lucas akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo, amewaonya wanaofanya matukio ya wizi mtaani hapo kuacha mara moja na endapo wataendelea wakiwakamata wataendelea kuwashughulikia.