Storm FM

Serikali za mtaa zaongoza malalamiko ya rushwa Geita

1 February 2025, 1:26 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Geita kwa mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka 2024 imepokea jumla malalamiko 43, makosa ya rushwa yakiwa ni 32 na yasiyohusu rushwa yakiwa 11.

Na: Daniel Magwina – Geita

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita Azza Mtaita ameeleza hayo Januari 31, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya mwenendo wa makosa mbalimbali.

Waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa TAKUKUKURU Geita. Picha na Daniel Magwina

Mtaita amesema idara zilizo lalamikiwa na wananchi ni serikali za mitaa malalamiko 7,elimu 4,utawala 5, afya 6,mahakama 2, fedha 2,nishati 2,ujenzi 4,sekta binafsi 1,vyama vya ushirika 2,ardhi 1,manunuzi 3,madini 1,mifugo 1,usafirishaji 1 na tasaf 1.

Sauti ya mkuu wa TAKUKURU Geita

Mkuu wa TAKUKURU ameongeza kuwa malalamiko 32 uchunguzi wa awali umeshawasilishwa na malalamiko 11 walalamikaji wake wameeimishwa na kupewa ushauri.