Storm FM

Mzozo waibuka Geita baada ya Yanga kufurushwa klabu bingwa

20 January 2025, 2:15 pm

Logo za vilabu vya Yanga SC na Simba SC . Picha kutoka mtandaoni

Baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu ambao hawajafahamika majina yao katika halmashauri ya manispaa ya Geita wameingia katika ugomvi na majibizano kwa kile kilichodaiwa ni ushabiki wa timu zao za Simba na Yanga

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Chanzo cha ugomvi huo kinaelezwa kuwa Januari 18, 2025 baada ya mechi ya Yanga SC dhidi ya MC Alger kukamilika kwa droo ya sare ya bila kufungana hatua iliyofanya klabu ya Yanga kuaga mashindano ya Klabu bingwa barani Afrika ndipo mashabiki wa  Simba wakaanza utani wa kurusha maneno.

Sauti ya majibizano

Mmoja wa  mashuhuda aliyekuwepo katika eneo hilo John Mgeta ameeleza kuwa hali ya utani wa jadi si kosa, bali watu waweke mipaka katika utani huo ili kuondoa migongano.

Sauti ya shuhuda

Ugomvi huo ulitokea katika kijiwe cha kahawa ambapo mwenyekiti wa kijiwe hicho ambaye pia hakutaka kutaja jina lake ametoa rai kwa mashabiki wa soka kuelewa dhana ya utani wa jadi na sio kuweka hasira.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiwe