Baba mkwe adaiwa kumtaka kimapenzi mkwe wake Geita
15 January 2025, 10:48 am
Migogoro ya kifamilia bado ni changamoto kwa baadhi ya maeneo hali ambayo imekuwa ikikwamisha jitihada za utafutaji.
Na: Kale Chongela – Geita
Mwanamke Kabula Makelemo (21) mkazi wa mtaa wa Mpomvu kata ya Mtakuja Manispaa ya Geita amejikuta katika wakati mgumu baada ya baba mkwe wake kumtaka arudi kwao baaa ya mume wake kusafiri huku sababu ikiwa haijabainishwa.
Akizungumza Januari 13, 2025 na Stom FM Bi. Kabula amesema kumekuwa na mfululizo wa hali ya ugomvi na kutoelewana na baba mkwe wake kwa kipindi ambacho mume wake hayupo.
Mama mzazi wa mwanamke huyo Tekla Mashiri ameeleza kuwa chanzo cha mgogoro katika familia ya mtoto wake ni baba mkwe kuingilia ndoa hiyo kwa kuwachonganisha huku akimtaka kimapenzi.
Kufuatia malalamiko hayo baba mkwe ambaye anafahamika kwa jina la John Petro amesema kuwa alimwambia aondoke nyumbani hapo asubiri mumewe atakapo rudi na kukanusha tuhuma za kuhusishwa kuwa amemtaka kimapenzi.
Mgogoro huo umefika hadi ofisi ya serikali ya mta wa Mpomvu kata ya Mtakuja na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo amefafanua namna ambavyo ametatua mgogoro huo.