Storm FM

Watoto wanaokimbilia mitaani tishio Geita

8 January 2025, 10:45 am

Sehemu ya jengo la ofisi ya serikali ya mtaa wa Nyerere road mjini Geita. Picha na Mrisho Sadick

Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali za kuhimiza wazazi kuzingatia malezi ya watoto na kuhakikisha hawatoroki kutoka majumbani kwenda mitaani, bado imekuwa ni changamoto katika mtaa wa Nyerere road Geita mjini.

Na: Ester Mabula – Geita

Wananchi wilayani Geita wameiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuwarejesha makwao watoto wanaoishi mtaani kwani kundi hilo kwasasa limegeuka tishio kwa kuanza kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi wa mali za watu.

Wakizungumzia changamoto hiyo Januari 06, 2025 baadhi ya mama lishe katika ofisi ya mtaa wa Nyerere road mjini Geita baada ya kuwakamata watoto wawili wanaoishi mtaani wenye umri kati ya miaka 12 na 13 waliowaibia masufuria zaidi ya 10 nakwenda kuyauza kama vyuma chakavu huku wakiiomba serikali kuchukua hatua za haraka kuepusha hatari zaidi siku za usoni.

Sauti ya mama lishe
Baadhi ya vyombo vya mama lishe vilivyoibwa na watoto waliokamatwa mtaa wa Nyerere road mjini Geita

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere road Dua Issa ametoa onyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaowatumikisha watoto hao kwenye kazi zao hali ambayo inawafanya kuendelea kuongezeka.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa
Watoto waliokamatwa wakiiba vyombo vya mama lishe katika mtaa wa Nyerere road mjini Geita

Mtendaji wa mtaa huo George Maguga amesema watoto waliokamatwa kwa wizi wa sufuria wametoa Serengeti Mkoani mara na mwingine ametoka Ngara Mkoani Kagera nakwamba kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi na ustawi wa jamii wameendelea kuwakamata nakuwapeleka makwao.

Sauti ya mtendaji wa mtaa