Storm FM

Mtoto (8) adaiwa kubakwa kwa jirani Geita

6 January 2025, 10:53 am

Mtoto anayedaiwa kufanyiwa ukatili wa kubakwa baada ya kwenda kuangalia TV kwa jirani. Picha na Edga Rwenduru

Licha ya serikali, wadau na wanaharakati wa haki za binadamu kuendelea kukemea vikali juu ya matukio ya ukatili, bado vitendo hivyo vinaendelea kujitokeza huku waathirika wakiwa ni watoto.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 mkazi wa mtaa wa Lwenge kata ya Kalangalala katika Manispaa ya Geita mkoani Geita anadaiwa kubakwa na kijana mmoja ambaye ni jirani yake baada ya mtoto huyo kwenda kutazama TV kwenye chumba cha mtuhumiwa huyo.

Nyumba anayoishi mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto wa miaka 8. Picha na Edga Rwenduru

Tukio hilo limetokea Januari 04, 2025 akizungumza kwa masikitiko babu wa mtoto huyo anasema familia ilianza kuhisi kuna jambo lisilo la kawaida baada ya mtoto huyo kuanza kutembea kwa shida na walipomhoji alikiri kufanyiwa ukatili na kijana huyo.

Sauti ya babu wa mtoto
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Geita Yohana Mlole. Picha na Edga Rwenduru

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Geita Yohana Mlole amethibitisha kumpokea mtoto huyo na kumfanyia vipimo ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alichukuliwa na Jeshi la polisi kwaajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.

Sauti ya daktari

Balozi wa eneo hilo pamoja na Kamanda wa polisi jamii wanaeleza namna ambavyo walipata taarifa ya tukio hilo.

Sauti ya balozi na kamanda wa polisi jamii

Baadhi ya majirani wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Sauti ya majirani