Storm FM

Nyani tishio kwa wakazi mtaa wa Nyanza

30 December 2024, 10:48 am

Baadhi ya nyani wakiwa katika makazi yao katika mtaa wa Nyanza. Picha na Evance Mlyakado

Kwa zaidi ya miaka sita imeelezwa kuwa nyani waliopo katika mtaa wa Nyanza mjini Geita wameendelea kuleta changamoto ikiwemo udokozi wa vitoweo kwa wakazi wa eneo hilo.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Wakazi wa mtaa wa Nyanza, eneo la Kagera, kata ya Kalangalala mjini Geita wamelalamikia uwepo wa nyani ambao wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa ikiwemo uharibifu wa mazao ya kilimo na vitu vya ndani vya wananchi.

Wakizungumza na wanahabari Disemba 28, 2024 wananchi hao wameelezea changamoto wanazokumbana nazo kutokana na uwepo wa nyani hao huku wakidai wanashindwa kuwadhibiti kutokana na kuwa nyani ni miongoni mwa nyara za serikali.

Sauti ya wananchi
Sehemu ya mazao yaliyoharibiwa na nyani katika mtaa wa Nyanza mjini Geita. Picha na Evance Mlyakado

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyanza, Deogratius Kazili amesema kero ya nyani imekuwa ya muda mrefu huku akitoa wito kwa mamlaka husika kushughulikia suala hilo mara moja.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa

Afisa mifugo wa halmashauri ya mji wa Geita Bw. Lee Kihangala amesema shughuli ya kuwakusanya nyani hao imeanza ambapo nyani wapatao 163 wameondolewa na kupelekwa katika hifadhi ya Moyowosi iliyopo mkoani Kigoma.

Sauti ya Afisa mifugo