Storm FM

Wasiojulikana wavamia na kuharibu mazao shambani Kanyala

18 December 2024, 2:28 am

Muonekano wa shamba mara baada ya watu wasiojulikana kuharibu mazao baada ya kuvamia. Picha na Kale Chongela

Katika hali ya kushangaza watu wasiojulikana wamevamia na kufanya uharibifu wa mazao katika shamba lenye ukubwa wa ekari mbili.

Na: Kale Chongela – Geita

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Mkangala kata ya Kanyala halmashauri ya mji wa Geita  ambapo kwa mujibu wa mmiliki wa shamba hilo Bw. Ludovick Aloyce ameeleza kuwa tukio hilo limefanyika usiku wa kuamkia Disemba 17, 2024.

Sauti ya mmiliki wa shamba
Bw. Ludovick Aloyce akiwa amesimama katika shamba lake mara baada ya uharibifu kufanyika. Picha na Kale Chongela

Afisa mtendaji wa kata ya kanyala Bw. Mpanduji Charles amethibitisha kutokea kwa uharibifu huo na kueleza kuwa jitihada zinaendelea ili kubaini aliyehusika na uharibifu huo ili achuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria .

Sauti ya afisa mtendaji wa kata

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mkangala Bw. Abely Koronely ameeleza changamoto za namna hiyo zimekuwa zikijitokeza ambapo zinahusisha migogoro ya kuuziana maeneo.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa

Baadhi ya wananchi ambao ni wakazi wa mtaa huo akiwemo mtoto wa mmiliki wa shamba wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuombawatu kuacha kujichukulia maamuzi ambayo yanapelekea uharibifu na hasara.

Sauti ya wananchi