Wananchi mtaa wa Shilabela walia wimbi la vibaka
14 December 2024, 10:57 am
Uwepo wa vitendo vya wizi wa mali umeendelea kuwa mwiba kwa wakazi wa mtaa wa Shilabela kata ya Buhalahala mjini Geita ambapo wananchi wameeleza adha wanayopitia.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Wananchi wa mtaa wa shilabela kata ya Buhalahala halmashauri ya mji Geita wamelalamikia kuongezeka kwa matukio ya wizi na uporaji wa mali zao unaofanywa na vijana wadogo jambo ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Baadhi ya wananchi hao wamesema kwa sasa wanaishi kwa wasiwasi mkubwa wakiofia mali zao kuibiwa ikiwemo mifugo pamoja na mali za ndani licha ya jitihada zinazofanywa na ofisi ya mtaa huo kwa kushirikiana na Polisi jamii kuweza kudhibiti matukio ya wizi na uporaji
Wakizungumza baadhi ya vijana waliokamatwa katika ofisi ya polisi jamii mtaa wa Shilabela wamesema wapo kikundi ambacho kina zaidi ya vijana 20 wanaozunguka katika mitaa mbalimbali kwaajili ya kutekeleza matukio hayo ya wizi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Shilabela Fredrick Masalu amesema vijana wengi wanaofanya matukio hayo ni watoto wanaoishi mitaani baada ya kutoroka majumbani kwao.