Storm FM

Mpangaji aezuliwa paa kwa kushindwa kulipa kodi Geita

6 December 2024, 9:57 am

Muonekano wa nyumba upande ambao bati limeondolewa na mwenye nyumba kwa kushindwa kodi kwa wakati. Picha na Paul William

Janeth Thomas mkazi wa mtaa wa Buchundwankende kata ya Nyankumbu halmashauri ya mji wa Geita amebaki njia panda baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuezuliwa paa na mwenye nyumba wake kwa madai kuwa hajalipa kodi ya kwa muda wa miezi mitano.

Na: Paul William – Geita

Tukio hilo limetokea siku ya jumanne Disemba 03, 2024 024 wakati mama huyo akiwa kwenye biashara yake ambapo inadaiwa mwenye nyumba alifika katika nyumba hiyo na kijana aliyemtumia kupanda juu ya nyumba upande wa chumba cha mpangaji wake na kuanza kung’oa bati.

Akizungumzia tukio hilo Bi. Janeth amesema maamuzi hayo yamepelekea uharibifu wa baadhi ya vitu vilivyoko ndani kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Sauti ya mpangaji

Menye nyumba Bi. Zamda Edward ambaye ni mkazi wa Nyankumbu akizngumza na Storm FM amekiri kufanya tukio hilo kwa madai ya kucheleweshewa kodi yake ya nyumba na mpangaji huyo.

Sauti ya mwenye nyumba na mwandishi
Muonekano wa nyumba upande ambao bati limeondolewa na mwenye nyumba kwa kushindwa kodi kwa wakati. Picha na Paul William

Mwenyekiti wa mtaa wa Buchundwankende Hassan Ally Nkwandwe amesema taarifa za kuezuliwa kwa paa hazijafika ofisini kwake bali mpangaji huyo kipindi cha nyuma amewahi kupeleka malalamiko ya kufungiwa nyumba na mwenye nyumba wake.

Sauti ya mwenyekiti Hassan Ally