Storm FM
Picha: Wananchi Geita mjini washiriki uchaguzi serikali za mitaa
27 November 2024, 10:39 am
Leo Novemba 27, 2024 wananchi nchini Tanzania wanashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwaajili ya kuchagua viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Na: Ester Mabula – Geita
Baada ya mabadiliko ya kikatiba na kuruhusiwa kwa vyama vingi, uchaguzi wa kwanza wa serikali za mitaa ulifanyika mwaka 1999. Uchaguzi huu ulifanyika kwa mara ya kwanza katika mazingira ya ushindani wa kisiasa, ambapo vyama vya upinzani vilishiriki.
Baada ya uchaguzi wa mwaka 1999 ukafatia 2004 kisha 2009, 2014, 2019 na leo utakuwa ni uchaguzi wa 6 kufanyika kwa mwaka huu 2024.