Upepo waezua nyumba Geita
20 November 2024, 9:14 pm
Halmashauri ya mji wa Geita imeendelea kukumbwa na majanga baada ya siku chache kupatwa na mafuriko sasa upepo mkali waezua nyumba.
Na Kale Chongela:
Mvua iliyoambatana na upepo Mkali imeezua jengo la ukumbi wa mpira na vibanda vinne vya wafanyabiashara katika mtaa wa Nyantorotoro A Kata ya Nyankumbu Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita.
Tukio hilo limetokea novemba 19 ,2024 huku baadhi ya wahanga wa tukio hilo wameiambia Storm FM Kuwa upepo huo ulikuja ghafla baada ya kunyesha mvua kubwa kwa muda mfupi nakusababisha uharibifu mkubwa kwenye vibanda hivyo.
Diwani wa kata ya Nyankumbu Mhe John Lunyaba Mapesa amethibitisha kutokea kwa uharibifu huo katika eneo lake na kueleza kuwa hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyotokea huku akiwasisitiza wananchi kujenga nyumba zao kwa ubora kuepuka majanga.