GGML kuendelea kufadhili miradi kupitia CSR
14 October 2024, 11:54 am
Mkoa wa Geita umeendelea kujivua uwepo wa mgodi wa GGML kwa kuwa umekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi katika nyanja mbalimbali hususani katika sekta za elimu na afya.
Na: Ester Mabula – Geita
Mgodi wa GGML umeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kutekeleza miradi ya maendelea kupitia sera ya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR).
Akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Oktoba 13, 2024 katika hafla ya ufungaji wa maonesho ya saba ya kitaifa ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini makamu wa Rais mwandamizi wa Anglo Gold Ashant Afrika Terry Strong amesema Kupitia CSR, GGML inatenga zaidi ya shilingi Bilioni 9 kila mwaka kwaajili ya kuwekeza katika elimu, afya, miundombinu, namiradi ya kuongeza kipato ili kuboresha maisha.
“Kulingana na ripoti ya TEITI ya hivi karibuni, GGML ilichangia asilimia 31.7 ya michango yote ya CSR kwenye sekta ya madini, na kuufanya mgodi huo kuwa mchangiaji mkubwa zaidi wa CSR.
GGML imejikita katika kuunda ajira, kujenga ujuzi, na kuinua uchumi wa ndani na kwamba kwa sasa wana ajira zaidi ya watu 6,900 wakiwemo wakandarasi, ambapo asilimia 98 ni Watanzania na zaidi ya asilimia 80 wakiwa katika nafasi za uongozi wa juu” – amesema Terry Strong.
Rais Samia amesema serikali itaendelea kuwekeza kwa wachimbaji wadogo na kwamba wamenunua mitambo 15 ya kuchoronga miamba kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ameomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kubadilisha jina la uwanja wa maonesho ya EPZA na kuuita “Uwanja wa maonesho wa Samia.”