Storm FM

Mkurugenzi Geita mji akagua vituo vya uandikishaji

11 October 2024, 2:02 pm

Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi akizungumza na Storm FM. Picha Kale Chongela

Leo Oktoba 11, 2024 limezinduliwa rasmi zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Na: Kale Chongela – Geita

Mkururgenzi mtendaji wa halmashauri mji wa Geita Ndugu Yefrerd Myenzi amewataka wananchi kutumia siku kumi zilizopagwa kujitokeza na kujiandikisha katika daftari la makazi.

Myenzi amesema hayo baada ya kukagua kituo cha uandikishaji katika mtaa wa Nyanza kata ya Kalangalala mjini  Geita leo oktoba 11 akisisitiza kuwa kujiandikisha katika daftari la makazi itamuwezesha mwananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sauti ya Mkurugenzi Yefred Myenzi

Diwani wa kata ya Kalangalala Prudence Temba amesema miongoni mwa sifa kuu ya kushiriki katika uchaguzi ni kuhakikisha jina la mwananchi limeandikwa kwenye daftari la makazi.

Sauti ya Diwani
Zoezi la uandikishaji likiendelea kwa baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kituo cha Nyanza. Picha na Kale Chongela

Baadhi ya wananchi kutoka halmashauri ya mji wa Geita ambao wameshiriki zoezi la uandikishaji katika daftari la makazi wamebainisha kuwa nafasi hii ya wao kujiandikisha inawapa wigo mpana wa kuchagua viongozi wanaofaa.

Sauti ya wananchi