Wananchi Geita wahimizwa kuhakiki mizani kabla ya kununua
10 October 2024, 11:57 am
Wakala wa vipimo nchini Tanzania wameendelea kutoa elimu juu ya vipimo sahihi kwa wananchi na wafanyabiashara ili kuondoa changamoto mbalimbali.
Na: Ester Mabula – Geita
Kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Geita amesema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maonesho ya 7 ya teknnolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita hivyo amewahimiza wananchi kufika katika banda lao ili kupata elimu zaidi.
Ameeleza kuwa ni muhimu mfanyabiashara au mwananchi anayetaka kuanza biashara kuhakiki mzani anaonunua uwe na nembo ambayo imehakikiwa ili kuondoa changamoto na migongano inayoweza kujitokeza.
Katika hatua nyingine amewasihi wananchi wanaopima uzito kwa watu wanopita mtaani kujiridhisha na mizani wanayotumia ili kupata majibu sahihi.
Maonesho ya 7 ya teknlojia ya madini yanaendelea mkoani Geita ambapo yalianza Oktoba 02, 2024 na yanatarajiwa kufungwa Oktoba 13, 2024 amabapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.